KELL BROOK KUVAANA NA GENNADY JUMAMOSI HII

MWANAMASUMBWI wa Uingereza, Kell Brook anatarajiwa kupanda ulingoni kutoana jasho na Gennady Golovkin.

Pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu limepangwa kupigwa katika uzito wa kati Jumamosi hii katika jiji la London.

Brook ambaye ndie bingwa wa uzani wa unyoya, anaruka mizani miwili ili kukabiliana na Golovkin ambaye ameshinda mapigano yake yote kwa njia ya “Knockout”.

Bingwa wa zamani wa uzani wa Welter duniani Sugar Ray Leonard alirudi katika uringo wa masumbwi mwaka 1987 baada ya kustaafu na kumshinda bingwa wa uzani wa kati wa wakati huo, Marvin Hagler.

“Nataka kufanya kile ambacho Leonard alifanya na Hagler, nitatumia kasi namiguu yangu kumkabili Golovkin,” alisema Brooks.


“Ninamuogopa kwa kweli, najua ni mrushaji wa makonde mazito na ndio sababu hakuna mtu anayetaka kupigana nae. Lakini hofu hiyo inanipa motisha kwa sababu itanifanya niwe mwangalifu zaidi na kuwa kama paka.”

No comments