KIGOGO SLOVENIA KUMRITHI MICHAEL PLATINI UEFA

IMERIPOTIWA kuwa rais wa chama cha soka cha Slovenia Aleksander Ceferin yuko mbioni  kuliongoza shirikisho la soka la Ulaya (UEFA).

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Uingereza la (BBC), Ceferin ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwania kiti cha urais katika Uefa, tayari ana uhakika wa kura 40 katika nchi 55 wanachama wa shiirikisho hilo.

Ceferin anaachana na Mholadhi Michael Van Praag katika mbio za kuwania cha urais kilichoachwa na Michael Platini.


Platini amefungiwa kijishughulisha na masuala ya mchezo wa soka kwa kipindi cha miaka minne kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

No comments