KING BLAISE ASEMA YEYE NDIYE MAKAMU WA RAIS WA FM ACADEMIA


MWIMBAJI mwenye sauti ya kipekee King Blaise wa FM Academia (pichani kulia), amesema yeye ndiye makamu wa rais wa bendi hiyo chini ya rais Nyoshi el Saadat.

Akiwa kwenye jukwaa la kundi la Mapacha Music Band, alipokuwa amepanda kusalimia kisanii, King Blaise akaweka hadharani cheo chake.

“Mimi ndiye makamu wa rais wa FM Academia na nimesimama hapa kutoa salam rasmi za FM Academia kwaajili ya kumpongeza Jose Mara kwa namna anavyoendeleza jahazi la Mapacha Music Band,” alisema King Blaise ndani ya ukumbi wa Meridian Hotel Jumapili iliyopita.

No comments