KIPIGO CHA WATFORD CHAYEYUSHA USINGIZI WA MOURINHO... asema hamasa kwa wachezaji wake ilikuwa ndogo

MATOKEO mabaya dhidi ya Watford yanaendelea kumnyima usingizi kocha Jose Mourinho ambapo sasa analia na hamasa ya wachezaji wake.

Kikosi cha Jose Mourinho kiliambulia kipigo dhidi ya Watford baada ya kufungwa mabao 3-1.

Haya ni matokeo mengine mabaya kwa Manchester United katika kipindi cha siku nane.

Hata hivyo, Mourinho amesema kuwa timu yake ndio iliyokuwa bora na ingefaa kujipatia ushindi lakini hamasa kwa wachezaji ilikuwa ndogo.

“Kitu ninachoweza kusema ni kwamba timu ilikosa hamasa ingawa tulicheza vizuri.”


“Ninaingia kazini nikitambua kuwa kuna tatizo ambalo lazima lifikie tamati kwa timu kuanza kupata ushindi na pointi tatu katika kila mechi,” alisema Mourinho.

No comments