KIUNGO WA WATFORD AMKINGIA KIFUA POGBA DHIDI YA LAWAMA ZA KUTOFANYA VYEMA

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama anaonewa, kiungo wa Watford, Roberto Pereyra amemkingia nyota mwenzake wa zamani wa Juventus, Paul Pogba kwa kusema kuwa ana kila kitu cha kubadilisha mchezo.

Pereyra jana alikutana na Mfaransa huyo wakati Manchester United ilipokwenda Vicarage Road na staa huyo anasema kuwa anamfahamu vizuri nyota mwenzake huyo.

Vinara hao wawili walicheza pamoja kwa muda wa miaka miwili kwenye klabu hiyo ya mjini Turin kabla ya wote kuhamia England na sasa Pereyra ana matumaini staa mwenzake huyo atakuja kung’ara tena.

“Ni mchezaji mahiri,” Pereyra aliliambia gazeti la The Guardian.

“Ana kila kitu na ana kila aina ya ujuzi. Ni kati ya wachezaji waliowahi kunishangaza wakati nilipokutana nae kwa mara ya kwanza,” aliongeza staa huyo.


Alisema kuwa kwa sasa anashangazwa na lawama zinazoelekezwa kwa nyota huyo baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi zake za kwanza.

No comments