KLOPP ASALENDA KWA DANIEL STURRIDGE… aanza kumbembeleza na kusema wataelewana tu

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp ni kama anaonekana kumbembeleza nyota wake Daniel Sturridge baada ya kusema kwamba wataelewana licha ya kumsugulisha benchi wakati wa mechi ya mwisho dhidi ya Tottenham.

Wakati wa mchezo huo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa White Line na kumalizika kwa sare ya 1-1, staa huyo wa timu ya taifa ya England alionekana kukerwa na kitendo cha kukalishwa benchi kabla ya kupangwa dakika za mwisho.


Sturridge alipangwa pembeni katika mchezo ambao walifungwa na Burneley lakini akawekwa benchi baada ya staa mwingine Sadio Mane kurejea uwanjani.

No comments