KOCHA DAVID MOYES AMTAKA LAMINE KONE ABAKI SUDERLAND

LAMINE Kone atafanya mazungumzo na klabu yake ya Sunderland kuhusu mkataba mpya na kocha David Moyes ameshasema kwamba lazima mchezaji huyo abaki.

Sunderland ilitupiliambali kitita cha pauni mil 20 kutoka Everton mwishoni kabisa mwa dirisha dogo la usajili kwa ajili ya mchezaji huyo kutoka Ivory Coast kwa akili ya kupigania namba katika dimba la Goodison Park.
Lakini sasa Moyes amesema kwamba hataki kumwachia mchezaji yeyote kuondoka ikiwa ana uwezo mkubwa.
“Hakuna ambacho kimejificha kwangiu kwa Lamine, ni mchezaji mzuri sana anajua kufanya kazi yake wakati wote,” amesema Moyes.


“Kwangu ilikuwa vigumu kumwachia. Nawezaje kumwachia mtu ambaye najua umuhimu wake. Sijawa na tabia hiyo bado. Mimi ni kocha ninayejali wachezaji,” amesema.

No comments