KOCHA EVERTON ATAJA SIRI YA USHINDI WAO DHIDI YA MIDDLESBROUGH

KOCHA wa Everton, Ronald Koeman ametaja siri ya ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Middlesbrough akisema kuwa kitendo cha mwamuzi Lee Mason kukubali bao la kujifunga lililowekwa kimiani na mlinda mlango wao, Maarten Stekelenburg baada ya kugongana na straika wa timu pinzani, Negredo ndicho kilichowarejesha katika mchezo na kisha wakaondoka na ushindi huo.  

Katika mchezo huo wa juzi, Stekelenburg aliusukumia nyavuni mpira ikiwa ni dakika ya 21 baada ya kugongana na Negredo lakini Mason akaona mshambuliaji huyo raia wa Hispania hakufanya madhambi.

Bao hilo la kujifunga la Mholanzi huyo kiuliifanya Everton kuzinduka na kisha ikafanikiwa kufunga mabao matatu kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wao, Gareth Bale, Seamus Coleman na Romelu Lukaku.

“Ilikuwa sio siku mbaya. Mwanzo hatukuanza vizuri. Tulitakiwa kuwa makini na hatukutakiwa kusubiri makosa ya mwamuzi,” Koeman aliuambia mtandao wa BT Sport.

“Baada ya makosa hayo, tulishuhudia Everton ilivyozinduka. Tulicheza soka zuri na kipindi cha pili nadhani tuliudhibiti mchezo,” aliongeza kocha huyo.

No comments