KOCHA JUVENTUS ASEMA BADO ANA MATUMAINI YA KUTUSUA LIGI YA MABINGWA

KOCHA wa Juventus, Massimilliano Allegri amesema kwamba bado ana matumaini watafanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabigwa licha ya kwenda suluhu na Sevilla.

Mabingwa hao wa Ligi ya Serie A usiku wa kuamkia juzi walipata nafasi nyingi wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini wakashindwa kuzitumia.

Hata hivyo, Allegri ameitaka timu yake kuwa na utulivu licha ya kushindwa kupata ushindi katika mechi yao ya kwanza ya Kundi H.


“Hakuna mechi rahisi katika michuano ya Ligi ya mabingwa hivyo lazima tusikate tamaa,” alisema kocha huyo kupitia katika tovuti ya klabu.

Tumefadhaika kwa kushindwa kupata pointi zote tatu, lakini bado tuna muda wa kuzinduka na tutaweza kutinga hatua ya 16 bora," aliongeza kocha huyo.

No comments