KOCHA MARTIN O’NEILL WA IRELAND AKANA KUWA MBIONI KUTUA HULL CITY

KOCHA wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Martin O’Neill amekanusha taarifa za kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Hull City inayoshiriki Ligi Kuu ya soka England (EPL).

O’Neill amekanusha uvumi huo alipohojiwa na vyombo vya habari mara baada ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.

“Sifikirii jambo lolote kuhusu uvumi huo.”

“Nipo hapa kwa makubaliano ya kimkataba na ninaheshimu suala hilo, kwa hiyo sitokuwa na mpango wa kufikiria kuondoka mpaka niweze kutimiza malengo niliyojiwekea katika timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland,” alisema O’Neill.

Jina la O’Neill limekuwa likitajwa miongoni mwa majina ya mameneja ambao wanapewa kipaumbele cha kuchukua nafasi ya Steve Bruce aliyetangaza kujiuzulu miezi mitatu iliyopita.

Kwa sasa kikosi cha Hull Citty kinanolewa na meneja wa muda, Mike Phelan ambaye ameonyesha kuwa na mtiririko mzuri wa matokeo tangu kuanza kwa msimu huu kufuatia matokeo ya sare mbili na ushindi mara moja.

Kocha huyo amesema ni vyema kila anayetaka kutoa taarifa zinazomhusu yeye awasiliane naye mapema ili kuepuka kutoa taarifa zisizo sahihi.


“Mimi ni kocha na ambaye naweza kwenda mahali popote, lakini ni vyema nikawa na muda wa kutafakari vyema a nikapewa uhuru huo baada ya kusingiziwa,” amesema. 

No comments