KOCHA PEP GUARDIOLA AMTABIRIA MAKUBWA AGUERO

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kwamba Aguero anaweza kufanya makubwa zaidi licha ya kuuanza vyema msimu huu.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Argentina alizikosa mechi tatu baada ya kufungiwa kwa kosa la kumpiga kiwiko beki Winston Reid wakati wa mchezo ambao Man City iliibuka na ushindi ya Westham United uliopigwa Agosti, mwaka jana, lakini pamoja na kuzikosa mechi hizo, straika huyo ameshafanikiwa kufunga mabao 11 katika mashindano yote.

Hata hivyo, pamoja na aguero kufungamabao mawili katika mechi ya Ligi Kuu ambayo waliibuka na ushindi dhidi ya Swansea City, Guardiola bado anaona kuna kitu ambacho staa huyo anatakiwa kukifanyia kazi.

“Sergio ana kiwango cha hali ya juu,” alisema kocha huyo. “Anafahamu kucheza vizuri akiwa ndani ya eneo la hatari na ndio mana ni mshambuliaji bora duniani, lakini nataka kumsaidia ili kuboresha soka lake.”


No comments