KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amesema mchezaji wake Diego Costa alichezewa rafu nyingi, jambo lililopelekea kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Swansea City.

Costa alichezewa rafu mara saba katika mchezo huo wakati yeye alicheza madhambi mara moja kwenye ,mechi hiyo ya Ligi Kuu England.
“Naweza kusema Diego Costa kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya 94 amechezewa rafu mara nyingi sana,” alisema Conte.

No comments