KOCHA WA ENGLAND 'KUTIMULIWA' BAADA YA KUDUMU MADARAKANI KWA MIEZI MIWILI ...gazeti lafichua uvundo kibao

Allardyce is fighting for his life as England manager after a sensational undercover sting
KOCHA wa England Sam Allardyce yupo kwenye hatari ya kupoteza kibarua chake kutokana na tuhuma zilizoibuliwa na gazeti la Daily Telegraph la nchini humo.
Uchunguzi wa gazeti la Daily Telegraph unasema kuwa Allardyce mwenye umri wa miaka 61,alitumia cheo chake kushauriana mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushauri kuhusu vile anaweza ''kuzunguka'' sheria za uhamiaji wa wachezaji.
Kwa mujibu wa Daily Telegraph, Allardyce maarufu kama Big Sam pia amelikosoa shirikisho la soka nchini Uingereza FA, kocha aliyemrithi Roy Hodgson, na msaidizi wake Gary Neville.
Allardyce yuko mazungumzoni na mwenyekiti wa FA Greg Clarke na afisa mkuu wa shirikisho hilo Martin Glenn katika kikao kinachoendelea kuwenye uwanja wa Wembley ambapo kuna hatari kubwa ya kocha huyo kutimuliwa kazi alichodumu nacho kwa miezi miwili tu.
Kama Allardyce atatimuliwa basi Gareth Southgate anaweza kuchukua nafasi yake kwa muda katika mechi zijazo dhidi ya Malta na Slovenia.  

No comments