KOLABO YA JOH MAKINI NA DAVIDO KUFUNGA MWAKA 2016

RAPA Janh Makini ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo "Perfect Combo" amesema ile kolabo yake pamoja na msanii kutoka nchini Nigeria, Davido anatarajia kuiachia mwishoni mwa mwaka huu.

John Makini alisema ushirikiano wa kazi na Msanii huyo aliutangaza muda mrefu sasa anaomba Mungu na kama kila jambo litakwenda sawa huenda mwishoni mwa mwaka huu akaachia kazi hizo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.


Alisema mara baada ya kutangaza ushirikiano huo mashabiki wake wengi walifurahia hivyo wakae mkao wa kula na mambo yakikamilika ndio utakaokuwa wimbo wa kufungia mwaka.

No comments