Habari

KUPAZA HUYOOO JUKWAANI TWANGA PEPETA MANGO GARDEN

on

ALIANZA kwa kum-miss Asha Baraka, lakini sasa ‘ameimiss’ na bendi yake
ya zamani – Twanga Pepeta – na hatimaye akaamua kwenda Mango Garden.
Huyo ni mwimbaji Saleh Kupaza ambaye wiki kadhaa zilizopita aliiambia
Saluti5 kuwa alimpigia simu ‘boss’ wake Asha Baraka baada ya kum-miss sana.
Jumamosi usiku, Kupaza anajitosa ndani ya ukumbi wa Mango Garden
kwenye show ya Twanga Pepeta majira ya saa 6 na nusu za usiku.
Ile anaingia tu ndani ya ukumbi, wimbo “Shida Darasa” ukawa hewani, Kalala
Jr akamwita jukwaani ili akaimbe wimbo huo alioshiriki kuutengeneza.
Bila hiyana Kupaza akapanda jukwaani na kilichofuata baada ya hapo ni
kelele za ushangiliaji za mashabiki wa Twanga Pepeta sambamba na kujazwa ‘mihela’
kwa mwimbaji huyo ambaye kwasasa anaitumikia Ivory Band.
Kupaza akiwa kwenye jukwaa la Twanga Peper Jumamosi usiku ndani ya Mango Garden

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *