LIVERPOOL WAIVAA TOTTENHAM VITA YA KUMPIGANIA LUCAS ALARIO WA RIVER PLATE

LIVERPOOL ya Jurgen Klopp wameingia katika kupigana vikumbo na Tottenham na kujikuta wote wakiwania saini ya mfumania nyavu wa timu ya River Plate, Lucas Alario.

Alario yupo katika kiwango cha juu cha soka kiasi cha kuziingiza vitani klabu hizo vigogo wa Ligi ya Premier.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 23 ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa wa nchini kwao, Argentina.

Hatua ya kuitwa kwake kucheza sambamba na Lionel Messi kumempa heshima ya hali ya juu ya kikosi na sasa anawindwa na timu kadhaa zikiwemo Liverpool na Spurs.

Liverpool wameweka mezani ofa ya pauni mil 12 ingawa klabu ya River Plate imebainisha dau la kuuzwa kwa Alario ni pauni mil 15.2.

Jarida la The Sun limeweka bayana azma ya kocha Jurgen Klopp kuvutiwa na straika huyo lakini hata hivyo ameweka mezani ofa ya pauni mil 8.5, fedha ambayo River Plate wanazikataa.


Pamoja na Liver na Spur, pia timu za Inter Milan na Torino za nchini Italia zimo katika mawindo ya saini ya Alario.

No comments