LIVERPOOL WALITUMA MASKAUTI KUMFUATILIA MAHMOUD DAHOUD

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp aliwatuma maskauti wake kumfuatilia kiungo mshambuliaji wa klabu ya Borussia Monchengladbach, Mahmoud Dahoud katika mtanange wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City wiki iliyopita.


Liverpool imepanga kiasi cha pauni mil 25 kwa ajili ya kumnasa Dahoud kwenye dirisha dogo la usajili wa Januari mwakani, huku kukiwa na ripoti za kwamba kinda huyo amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Monchengladbach.

No comments