Habari

LUIS NANI AMTETEA ROONEY KWA MOURINHO …ataka nahodha huyo wa United apewe nafasi

on

The Valencia winger enjoyed an eight-year spell at Old Trafford from 2007-2015
WINGA wa zamani wa Manchester United Luis Nani anaamini mchezaji mwenzake wa zamani Wayne Rooney anaweza kuimarika na kuwa mchezaji bora Old Trafford msimu huu. 
Hadi sasa hivi Rooney amefunga goli moja tu katika mechi saba na kuzua mjadala mkubwa iwapo anastahili kuwepo kwenye kikosi cha kwanza au aishie benchi.
Hata hivyo mchezaj huyo wa kimataifa wa England ambaye anahitaji magoli matatu tu  kufikia rekodi ya mabao 249 ya Sir Bobby Charlton ndani ya Manchester United, ametetewa na Nani anayekipiga na Valencia ya Hispania.
“Rooney ni mchezaji wa kipekee. Ana nguvu na mwenye kiwango kizuri, mfungaji, upeo na mwenye akili kubwa ya kuusoma mchezo,” Nani aliiambia Omnisport.
“Nilifurahia maisha kucheza nae pamoja. Ni mchezaji mwenye kubeba sehemu kubwa ya mafanikio ya Manchester United. Bado ana nafasi ya kujiimarisha na kutengeneza historia ya kipekee.”
Wayne Rooney continues to struggle for form at Manchester United this season
Wayne Rooney lawamani Manchester United
Manchester United manager Jose Mourinho has publicly backed his captain 
Jose Mourinho kocha wa Man United

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *