MAHAKAMA YA USULUHISHI KUAMUA MBIVU NA MBICHI YA SHARAPOVA MWEZI UJAO

MAHAKAMA ya usuluhishi wa migogoro ya michezo (CAS) imesema kuwa uamuzi wake juu rufaa ya Maria Sharapova kupinga kufungiwa miaka miwili utatangazwa wiki ya kwanza ya mwezi ujao.

Mshindi huyo mara tano wa michuano mikubwa ya "Grand Slam" alikata rufaa Juni mwaka huu siku chache baada ya shirikisho la Tenisi ulimwenguni kumfungia.

Mapema mwaka huu mrembo huyo raia wa urusi alitangazwa kufeli vipimo katika michuano ya Austirian Open.

Sharapova aligundulika kutumia dawa aina ya meldon hum ambazo alidai kuzitumia kwa ajili ya kuimarisha afya na si kwa lengo la kuongeza nguvu.


Kwa mara ya mwisho Sharapova alionekana uwanjani katika mashindano hayo ya Austaria Open ambapo alipoteza mcheza wa hatua ya robo fainali dhidi ya Serena Williams.

No comments