MAJERUHI LIONEL MESSI NJE WIKI TATU

KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa itakosa huduma ya nyota wao Lionel Messi kwa kipindi kisichopungua wiki tatu kutokana na maumivu ya nyonga.

Katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Atletico, staa huyo mwenye umri wa miaka 29 alilazimika kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Arda Turan.


“Leo Messi ana majeraha ya nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu,” ilisema taarifa iliyotolewa na Watukunya hao kupitia akaunti yao ya Twitter.

No comments