Habari

MAMADOU SAKHO AJIPALIA MKAA LIVERPOOL …amshutumu vikali kocha Jurgen Klopp

on

Mamadou Sakho has taken to Snapchat to express his frustration at a lack of playing time
MAMADOU SAKHO amejiweka kwenye hatari ya kutoichezea tena Liverpool baada ya ‘kumchamba’ kocha Jurgen Klopp kwenye mtandao wa Snapchat.
Beki huyo jana usiku akaonyesha kukerwa kwake na kusugulishwa benchi na Klop kwa kisingizio kuwa ni majeruhi.
Nyota huyo wa Kifaransa amesema yeye yuko fiti, amepona na anashangaa kwanini kocha wake anaendelea kudai bado anaumwa.
Sakho mwenye umri wa miaka 26 amesema ni wakati sasa wa mashabiki wa Liverpool kuelezwa ukweli badala ya taarifa za kizushi.
Baadhi ya vitu alivyoandika beki huyo ni: “Ni wiki tatu sasa tangu nipone, niko fiti na tayari kwa kucheza. Hawataki nicheze hata kwa timu ya pili, lol! Sijui ni kwanini.”
Liverpool manager Jurgen Klopp has not played Sakho for a single minute this season
Kocha wa Liverpool  Jurgen Klopp hajamchezesha Sakho hata kwa dakika moja msimu huu 
The French defender sprints during a training session at Melwood recently
 Sakho katika picha ya mazoezini hivi karibuni

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *