Habari

MAMBO SABA ANAYOSTAHILI KUYAFANYA MOURINHO ILI KUIOKOA MAN UNITED

on

Mourinho has publicly criticised his players but is thought to have been more vocal in private
MAMBO hayaendi kama yalivyotarajiwa kwa Jose Mourinho ndani ya
Manchester United.
Mshindi huyo wa mara mbili wa Champions League, alitarajiwa kuifanya
United iwe tishio kama ilivyokuwa enzi za Sir Alex Ferguson aliyestaafu ukocha
mwaka 2013.
Vipigo vya hivi karibuni kutoka kwa Manchester City, Feyenoord na
Watford, vimefichua baadhi ya mapungufu yaliyokuwepo tangu enzi za Louis van
Gaal aliyetimuliwa msimu uliopita.
Gazeti la The Sun la
Uingereza linaandika mambo saba ambayo Jose Mourinho anaweza kuyafanya ili kuifanya
United iwe tishio.
1. Kumpiga benchi Wayne Rooney
Manchester United and captain Wayne Rooney are struggling for form this season
Gazeti hilo linasema licha ya historia kubwa aliyonayo nahodha Wayne
Rooney kwa Manchester United, lakini uwezo mdogo anaouonyesha uwanjani hivi
sasa, unaididimiza timu.
The Sun linaandika kuwa
kumpiga benchi Rooney kutaleta uhai kwa Paul Pobga ambaye atakuwa na wasaa
mzuri wa kucheza nyuma ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
2. Kumrejesha Bastian Schweinsteiger kwenye kikosi cha kwanza
The midfielder has little prospect of first-team football in remaining two years of his contract
Siku zote Mourinho amekuwa
na tabia ya kuwatema baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa kwenye kila klabu
mpya aliyokwenda ili kuonyesha kuwa yeye ndiye ‘in charge’.
Ni mbinu nzuri na kumbukumbu zinaonyesha namna alivyokuwa akifanikiwa
kupitia mbinu hiyo, lakini United inakosa kiongozi kwenye eneo la kati.
Mourinho anapaswa kumrejesha kwenye kikosi cha kwanza kiungo mkongwe Bastian
Schweinsteiger ambaye uwezo wake si wa kubeza.
Si lazima aanze lakini anaweza kutokea benchi na kuisadia timu pale
itakapokuwa kwenye wakati mgumu.
Pobga aling’arishwa na viungo wakongwe wa Juventus, kitu ambacho
anaweza pia kufanyiwa na Schweinsteiger ndani ya Manchester United.
3. Kumuanzisha Marcus Rashford
Rashford celebrates scoring on his first league start of the season for Manchester United
Marcus Rashford ameonyesha uwezo wa hali ya juu ikiwa ni sambamba na
kufunga magoli muhimu, amekuwa akibalisha kasi ya timu kila anapoingia na ni
wazi kuwa anastahili kuanza katika kila mchezo hasa katika kipindi hiki ambacho
Anthony Martial amekuwa kwenye kiwango duni.
4. Kumpiga benchi David De Gea katika EFL Cup
Ander Herrera says goalkeeper David de Gea (pictured) always plays horrible music
Hakuna ubishi kuwa David De Gea ni mmoja wa makipa bora duniani,
lakini kitendo cha kuamini kuwa hagusiki na hana mpinzani Manchester United,
kimekuwa kikimfanya abweteke na kuzalisha makosa kadhaa yasiyostahili.
Mourinho anastahili kumipiga benchi katika baadhi ya mechi (hususan
mechi za EFL Cup) ili kumjengea changamoto ya ushindani, hatua itakayomfanya
kipa huyo wa Hispania ajitume zaidi.
5. Kumchezesha Morgan Schneiderlin
Tottenham had a move for midfielder Morgan Schneiderlin blocked by Manchester United
Huyu ni mchezaji mwingine ambaye hakufurahia maisha Old Trafford chini
ya Van Gaal – lakini ana vigezo vyote vya kuwa staa kwenye Premier League.
Wakati Mourinho anatwaa taji lake la mwisho akiwa na Chelsea, shujaa
wake alikuwa ni kiungo mkabaji Nemanja Matic.
Schneiderlin aling’ara sana akiwa na Southampton na anaonekana ni mtu
sahihi kwa aina ya soka la Mourinho.
Nidhamu yake ya mchezo, itamsadia sana kumpa uhuru Pogba ya kuzunguka
uwanja mzima.
6. Kusaka beki
mpya wa kulia
Antonio Valencia ameanza vema msimu na amekuwa akimudu nafasi ya beki
wa kulia tangu enzi za Sir Alex Ferguson, lakini amekuwa na makosa kadhaa
kwenye mchezo wake, hivyo Mourinho anahitaji beki shupavu atakayedhibiti
mashambulizi yote yanayotokea kushoto.
7. Kutoyaanika makosa ya wachezaji
Luke Shaw is said to be confused by Mourinho's differing approach to using full backs
Mourinho amemshutumu vikali beki Luke Shaw kwa kudai alihusika na ujio
wa baadhi ya magoli waliyofungwa na Watford.
Beki huyo wa kushoto amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu arejee
uwanjani msimu huu kufuatia kuvunjika vibaya mguu wake mwaka jana, hivyo
anahitaji kuungwa mkono na kocha badala ya kushutumiwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *