MAN UNITED YAFANYA MAUAJI KWA MABINGWA WATETEZI …Pobga atoa nuksi

Paul Pogba looked to the heavens after scoring his first Manchester United goal and their fourth of the afternoon
MANCHESTER UNITED imechomoza kucha zake na kuiadhibu vibaya Leicester City kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England.

Vijana wa Mourinho wakiwa nyumbani Old Trafford wakaibuka na ushindi wa 4-1 huku mabao yote ya wenyeji yakija katika kipindi cha kwanza.

Bao la kwanza la United lilikuja dakika ya 22 kupitia kwa beki Chris Smalling akiunganisha kwa kichwa kona ya Daley Blind.

Ikicheza bila nohadha wake Wayne Rooney, United ikaandika bao la pili dakika ya 37 Juan Mata baada ya gonga safi kati yake na Paul Pobga.

Dakika ya 40 mshambuliaji kinda Marcus Rashford akaendeleza makali yake kwa kuifungia United bao la tatu kabla Pobga hajafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Manchester United kunako dakika ya 42. Bao la Pobga nalo lilitokana na kona ya Blind.


Kipindi cha pili Mabingwa watetezi wakapata bao la kufutia machozi dakika ya 60 kupitia shuti kali la Demarai Gray.

Manchester United: De Gea; Valencia, Bailly, Smalling (c), Blind; Ander Herrera, Pogba; Lingard (Carrick 78), Mata (Young 87), Rashford (Rooney 83); Ibrahimovic

Leicester City: Zieler; Simpson, Morgan (c), Huth, Fuchs; Mahrez (King 46), Amartey, Drinkwater, Albrighton (Schlupp 62); Vardy (Gray 46), Slimani
The £89million signing lost Christian Fuchs and met Daley Blind's corner to send a header into the far corner
Pobga akiruka juu kufunga kupitia kona ya Daley Blind
Pogba soaks up the acclaim of the Old Trafford support after scoring his first goal since returning to the club
Pogba akishangilia mbele ya mashabiki Old Trafford 

No comments