MANCHESTER CITY YAJIPANGA KUMNYAKUA ALEXIS SANCHEZ

KLABU ya Manchester City imejipanga kuhakikisha inamnasa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez ambapo gazeti la The Sunday Express limedai kuwa City wanamfuatilia Mchile huyo anayemaliza mkataba wake na washika bunduki hao mwaka 2018 kwa ukaribu zaidi.


City watakuwa na furaha ya kumnasa Sanchez kwani wanaamini kuwa na uwezo wa kulipa mshahara anaoutaka Sanchez pale Arsenal ambao ni pauni 200, 000 kwa wiki.

No comments