Habari

MANCHESTER UNITED BADO KICHWA CHA PANZI …yapigwa 3-1 na Watford

on

LICHA ya kuanza Premier League kwa kishindo na
kushinda mechi tatu mfululizo chini ya kocha Jose Mourinho, Manchester United
imeanza kurejea kwenye enzi za kuchukua kichapo.
Timu hiyo imelambwa 3-1 na Watford katika mchezo
mgumu wa Premier League uliochezwa kwenye dimba la Vicarage Road.  
Huo unakuwa mchezo
wa pili mfululizo kwa United kupoteza katika Premier League baada ya kunyukwa
2-1 na Manchester City wikiendi iliyopita.
Lakini unakuwa
mchezo wa tatu mfululizo kupoteza katika mashindano yote kufuatia kipigo cha
1-0 kutoka kwa Feyenoord  kwenye Europe
League Alhamisi usiku.
Watford walikuwa wa
kwanza kuandika bao kunako dakika ya 34 kupitia kwa Etienne Capoue kufuatia
makosa ya mshambuliaji Anthony Martial aliyerejea nyuma kuokoa.
Mshambuliaji kinda
wa Manchester United Marcus Rashford akasawazisha dakika ya 62 na kuamsha ari ya
kusaka bao la ushindi.
Wakati United
wakipeleka mashambulizi mfululizo kwenye lango la Watford, wakajikuta
wanaruhusu bao la pili dakika ya 84 kupitia kwa Juan Camilo Zuniga huo
ukiwa ni mpira wake wa kwanza kuugusa baada ya kutokea benchi.
Dakika ya 90 Watford
wakapata penalti iliyopigwa na Troy Deeney na kuzaa bao la tatu.
Watford (4-4-2): Gomes 7; Cathcart 7, Britos 7.5, Prodl 8, Holebas 6.5; Janmaat 7 (Amrabat, 49, 7), Behrami 7, Capoue 7.5 (Zuniga 82), Pereyra 7; Deeney 7.5, Igahlo 6 (Success 90)
Manchester United (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 5.5 (Mata 62, 6), Smalling 5, Bailly 5.5, Shaw 6 (Memphis 85); Fellaini 5, Pogba 5; Rashford 7, Rooney 5, Martial 5 (Young 38, 6); Ibrahimovic 6
Etienne Capoue celebrates after scoring Watford's opening goal in the first-half at Vicarage Road
Etienne Capoue baada ya kuipatia Watford bao la kwanza

Rashford was in a hurry to get the match underway once again after scoring United's second-half equaliser
Rashford akishangilia baada ya kuisawazishia United
Juan Zuniga celebrates after scoring Watford's late second goal with his first touch after coming on as a substitute
Juan Camilo Zuniga  akishangilia bao lake

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *