MASANJA MKANDAMIZAJI ASEMA NDOA YAKE IMEFUNGUA NJIA KWA VIJANA

EMMANUEL Mgaya “Masanja Mkandamizaji” aliyefunga ndoa hivi karibuni na kuzua tafrani kwa wasanii wenzake kutiwa hatiani kwa kutumia sare za askari siku ya harusi yake na mkewe Monica Masatu, amefunga kwa kusema kuwa amefungua njia ya vijana wengi wenye maisha lakini hawataki kuoa.


“Unakuta kijana yuko safi kimaisha lakini hataki kuoa hela anayo kila kitu anacho na anakuwa na "burudisho" lakini kuoa hawataki sasa mimi nimewaonyesha njia sasa ole wake kijana mwenzangu asioe na kuwachezea mabinti nitatoa Displine,’’ alisema Masanja.

No comments