KUNDI zima la Mashauzi Classic chini ya Isha Mashauzi, Ijumaa hii litakuwa katika ukumbi wa New Chikaz ulioko Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Sumaragar ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni maalum kwa kufungua rasmi shughuli za burudani katika ukumbi huo mpya.

Waandaji wa onyesho hilo (New Chikaz) wameweka kiingilio cha shilingi 7000/= ili kuiona Mashauzi Classic.

“Onyesho limekodiwa na wenye ukumbi, sisi kazi yetu iliyobakia ni kwenda kutoa burudani ya nguvu kama ilivyo jadi yetu,” alisema Suma.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac