MASHAUZI KULA IDD MANGO, FM WAKO MEEDA, JAHAZI DAR LIVE, SIKINDE BULYAGA …pata ratiba ya bendi kibao


KUNDI kabambe la miondoko ya taarab Mashauzi Classic litahanikiza burudani zake ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni siku ya Eid el Hajj (Idd Mosi).

Wakati Mashauzi wakiwa Mango, maswahiba zao Jahazi Modern Taarab watakuwa pande za Mbagala ndani ya ukumbi wa Dar Live.

Miamba ya muziki wa dansi FM Academia watakuwa Meeda Club Sinza huku Twanga Pepeta wakipatikana Vijana Social Hall Kinondoni.

Kundi la Ogopa Kopa chini malkia Khadija Kopa litafanya onyesho lao la Idd Mosi kule Bunju kwenye ukumbi wa Sia Club huku Wakali Wao Modern Taradance wakiwapa raha wakazi wa Kilwa Masoko kwenye ukumbi wa By Night.

Ngoma kubwa Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” Idd Mosi watakuwa Bulyaga Bar Temeke huku mahasimu wao Msondo Ngoma Music Band na Malaika Band wakiipitisha Idd Mosi bila kufanya onyesho lolote.

Double M Plus ya kwake Mwinjuma Muumin “Kocha wa Dunia” itakuwa ndani ya ukumbi wa Villa Chamazi, wakati kundi la taarab la East African Melody likipatikana Lango la Jiji Magomeni.

Akudo Impact “Vijana wa Masauti” watakuwa kwenye ukumbi wao wa nyumbani Msasani Beach Club, Kawe lakini Talent Band ya Hussein Jumbe yenyewe itakuwepo Kisuma Mwembe Yanga.

Kundi zima la Tanzania One Theatre likiwa na TOT Taarab na TOT Band litajikita nyumbani kwao CCM Mwinjuma Mwananyamala wakati Mapacha Music Band chini ya Jose Mara wakiangusha burudani yao pande za Kimara Korogwe kwenye ukumbi wa Kinyange Bar.

Dar Modern Taarab nao watapatikana kwenye ukumbi wao wa nyumbani unaokwenda kwa jina la Dar Modern pale Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam.

Hizi ndiyo ratiba za bendi zetu zilizoifikia Saluti5. Kama tutapata nyongeza ya bendi nyingine tutaziongeza katika ukurasa huu huu. Pichani juu ni Akudo Impact.

No comments