MBINU ZA JURGEN KLOPP LIVERPOOL ZAMKUNA GEOGINIO WIJNALDUM

KIUNGO wa Liverpool, Georginio Wijnaldum anaonekana kukunwa na mbinu anazotumia kocha wao, Jurgen Klopp baada ya kusema kuwa kuna kitu maalum amekitengeneza na akasema kwamba anajivunia kuchezea klabu hiyo.

Kiungo huyo Mholanzi alitua kwenye klabu hiyo ya Anfield kabla ya dirisha la usajili halijafungwa akitokea timu iloiyoshuka daraja ya Newcastle United akiwa ameshafunga mabao 11 katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu England.

Licha ya nahodha huyo wa zamani wa PSV Eindhoven ambaye aling’ara katika mchezo ambao Liverpool waliondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea uliopigwa mwishoni mwa wiki kuwa hajafunga bao katika klabu yake mpya, lakini staa huyo mwenye umri wa miaka 25, anasema kuwa yapo mambo mengi yanakuja kutoka kwake kutokana na jukumu alilopewa na Klopp.

“Hiki ni kikosi chenye wachezaji wengi wenye vipaji na kocha mzuri,” Wijnaldum aliiambia tovuti ya Liverpool. “Nafikiri anajenga kitu maalum katika timu hii. Niliingiwa na wazo hilo wakati nilipokutana na Jurgen Klopp kwa mara ya kwanza.”


Alisema kwamba kwa sasa anafahamu hiyo ni klabu mbadala kwake na huku akisema kuwa anafurahi kuwa sehemu yake.

No comments