MESEN SELEKTA ADAI YEYE NDIE BINGWA WA KUREKODI SINGELI

MTAYARISHAJI wa muziki kutoka Studio ya Defatality, Mesen Selekta amefunguka na kusema kuwa yeye ndie mtayarishaji pekee anayetengeneza muziki halisi wa Singeli.

Akizungumza kwenye kipindi cha “The Base” cha ITV, Mensen alidai kuwa watayarishaji wengi wanajaribu lakini wanakosea kwa kufananisha muziki huo na Mnanda.

“Unajua kuna muziki unaitwa Singeli, kuna pia Mnanda na ladha tofauti. Wakati mwingine kuna baadhi ya watayarishaji wanajaribu kutengeneza Singeli lakini inakuwa sio Singeli kutokana na kuwa na midundo kama Mnanda,” alisema.


Alisema, hadi sasa yeye ndie aliyebaki kuwa mtayarishaji pekee wa Singeli nchini huku wengine wakijaribu kumfuatia lakini bado hawajafikia uwezo alionao.

No comments