MOURINHO AANZA VISINGIZIO KUJIHAMI NA KUUKOSA UBINGWA ENGLAND

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kaanza visingizio, kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa harakati zake za kutwaa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu zitavurugwa na michuano ya Ligi europa.

Usiku wa kuamkia juzi Man United ilikuwa ikikabiliana na vinara wa Ligi ya Uholanzi, Feyenoord katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya europa na huku Mourinho akitarajia kuwapunzisha nyota wake kama nahodha Wayne Rooney, Antonio Valencia na Luke Shaw ambao hawakwenda kwenye safari hiyo ya Rotterdam.

Hata hivyo Mreno huyo ambaye aliwahi kutwaa taji akiwa na FC Porto mwaka 2003, alisema kuwa ratiba ya sasa sio rafiki na harakati zake za kusaka taji la 21 la Uingereza.

“Ndio ni vigumu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kama unashiriki kwenye michuano ya Europaa,” alisema kocha huyo.

“Tungekuwa wazuri endapo tungepata nafasi ya kucheza Jumatatu ama Jumanne, lakini tunapocheza Alhamisi tunakuwa na siku moja ya kupunzika lakini hatuna nafasi hiyo,” aliongeza mreno huyo.

Alisema kuwa nafasi nzuri waliyonayo pekee ni kucheza na Liverpool siku ya Jumatatu, Alhamisi watakutana na Fenerbahce na kisha Jumapili watakutana na Chelsea.

No comments