MOURINHO AMSISITIZA POGBA "KUKAZA" ZAIDI UWANJANI

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama kamwambia bado hajaridhika, kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amemtaka staa wake, Paul Pogba kuonyesha makali yake licha ya kuiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Leister City katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo wa Jumamosi, staa huyo ambaye alisajiliwa kwa bei mbaya ndiye aliyeisaidia Manchester United kuondoka na ushindi huo ikiwa kwenye uwanja wake wa Old Trafford na huku akioneka kuwa katika kiwango kizuri kilichomfanya apate bao lake la kwanza akiwa na klabu hiyo.

Bao hilo la kichwa lilipatikana dakika ya 42 baada ya wachezaji Chris Smalling, Juan Mata na Marcus Rashford kumchambua mlinda mlango Ronrobert Zieler.

Hata hivyo pamoja na kupachika bao hilo, inaonekana kuwa bado kocha wake hajaridhika akimtaka kufunga mengi zaidi.

“Siwezi kufahamu kama hilo ndio soka lake tangu arejee kutoka Juventus lakini nadhani ameanza kucheza vizuri tangu tulipokutana  na Southampton na Hully City,” alisema Mourinho.

“Wakati timu inapocheza vibaya ni lazima na yeye atacheza vibaya, kama timu ikicheza vizuri na yeye atacheza vizuri,” Aliongeza Kocha huyo.


Alisema kwama anacho kitaka kwa sasa niu staa huyo na timu kucheza ili waweze kupata mafanikio makubwa.

No comments