Habari

MOURINHO NA GUARDIOLA VITANI TENA …NI MAN CITY NA MAN UNITED EFL CUP MZUNGUKO WA NNE

on

Jose Mourinho na Pep Guardiola wataingia tena vitani baada ya Manchester United kupangiwa kuumana na Manchester City katika mzunguko wa nne wa michuano ya EFL Cup.
Timu hizo zilikutana Septemba 10 kwenye uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ambapo City ilishinda 2-1.
Na sasa timu mmoja kati ya hizo italazimika kuaga EFL Cup pale zitakokutana mwezi Oktoba.
United imeishinda Northampton 3-1 katika mzunguko wa tatu wa EFL Cup huku City ikiibanjua Swansea 2-1.
Jose Mourinho and Pep Guardiola will meet again when United face City in the EFL Cup
Jose Mourinho na Pep Guardiola watakutana tena katika EFL Cup
MECHI ZA MZUNGUKO WA NNE
West Ham vs Chelsea
Manchester United vs Manchester City 
Arsenal vs Reading
Liverpool vs Tottenham 
Bristol City vs Hull City
Leeds United vs Norwich City
Newcastle vs Preston North End
Southampton vs Sunderland 
Mechi hizi zinatarajiwa kuanza kuchezwa Oct 24

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *