MOUSSA SISSOKO ADAI BLAISE MATUID KUWEKEWA ZENGWE NA PSG

STAA wa timu ya taifa ya Ufaransa Moussa Sissoko amesema kuwa staa mwenzake katika kikosi hicho Blaise Matuid alikuwa na mpango wa kwenda kutafuta changamoto mpya kwa kujiunga na Juventus lakini PSG ikamwekea kauzibe.

Kauli ya staa huyo imekuja baada ya mapema mwezi huu nyota huyo mwenye umri wa miakan 22 kukiri kuwa alitaka kukubali ofa kutoka kwa vinara hao wa Ligi ya serie A wakati wa majira haya joto lakini PSG wakamkatalia.

Kwa upande wake Sissoko yeye alilazimisha kuondoka Newcastle United lakini licha ya awali kuwa akihusishwa kwamba atajiunga na timu za Juve, PSG na Real Madrid, alijikuta akiangukia Tottenham zikiwa ni dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.


Na sasa kiungo huyo anasema kuwa yeye pamoja na Matuidi kila mmoja alikuwa akimuunga mkono mwenzake wakati wa michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya "Euro 2016" kuhusu kuzitema klabu zao ili wakatafute changamoto mpya.

No comments