MSONDO FAMILY DAY IJUMAA HII NDANI YA MANGO GARDEN


HATIMAYE lile onyesho  la Msondo Family Day la mwezi huu kupitia bendi ya Msondo Ngoma Music Band “Baba ya Muziki”  linafanyika Ijumaa hii ndani ya Mango Garden, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Onyesho hilo ambalo hufanywa kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, safari hii litafanyika Kinondoni baada ya kuunguruma katika wilaya za Ilala na Temeke.

Mmoja wa waratibu wa onyesho hilo, Abdulfareed Hussein, ameimbia Saluti5 kuwa maandalizi ya Msondo Family Day ndani ya Kinondoni tayari yako vizuri.
No comments