BAADA ya Msondo Ngoma kulingurumisha lile onyesho lao la Msondo Family Day katika wilaya za Temeke na Ilala sasa ni zamu ya wakazi wa Kinondoni.

Onyesho hilo ambalo hufanywa kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, safari hii litafanyika Mango Garden Kinondoni Ijumaa ya Septemba 30.

Mmoja wa waratibu wa onyesho hilo, Abdulfareed Hussein, ameimbia Saluti5 kuwa maandalizi ya Msondo Family Day ndani ya Kinondoni tayari yameshika kasi.

“Kwa kawaida kwetu sisi, linapoisha onyesho moja basi ndiyo mwanzo wa maandalizi ya onyesho linalofuata,” alitamba Abdulfareed.

Kama ilivyo ada, dhumuni la ‘Msondo Family Day’ ambayo hufanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, ni kuongeza mshikamano baina ya wanamuziki wa Msondo, mashabiki na wadau wakubwa wa bendi hiyo.

Abdulfareed ameongeza kuwa onyesho hilo maalum la kila mwezi, halitaishia Dar es Salaam pekee bali litafika hadi mikoani.

Mratibu huyo amesema zawadi mbali mbali za papo kwa papo ni sehemu ya Msondo Family Day.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac