ONYESHO lao la Msondo Family Day la mwezi huu kupitia bendi ya Msondo Ngoma Music Band “Baba ya Muziki”  ambalo litafanyika Kinondoni, linasubiriwa kwa hamu kubwa.


Onyesho hilo ambalo hufanywa kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, safari hii litafanyika Mango Garden Kinondoni Ijumaa ya Septemba 30.

Baada ya onyesho hilo kuunguruma katika wilaya za Ilala na Temeke, sasa wakazi wa Kinondoni wamepatwa na kiwewe cha furaha cha kushuhudia tukio hilo ndani ya eneo lao.

Mmoja wa waratibu wa onyesho hilo, Abdulfareed Hussein, ameimbia Saluti5 kuwa maandalizi ya Msondo Family Day ndani ya Kinondoni tayari yako vizuri.

Kama ilivyo ada, dhumuni la ‘Msondo Family Day’ ambayo hufanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, ni kuongeza mshikamano baina ya wanamuziki wa Msondo, mashabiki na wadau wakubwa wa bendi hiyo.

Hapo awali Abdulfareed alidokeza kuwa onyesho hilo maalum la kila mwezi, halitaishia Dar es Salaam pekee bali litafika hadi mikoani.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac