MUUAJI WA MANCHESTER UNITED AFANANISHWA NA DIEGO MARADONA

KOCHA wa Watford, Walter Mazzarri amesema kwamba bao lililofungwa na nyota wake, Troy Deeney wakati wa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Westham linamwonyesha kuwa na uwezo kama alivyokuwa nyota wa zamani wa Argentina, Diego Maradona.

Jana Watford walikuwa wakikaribisha kikosi cha Manchester United kwenye uwanja wao wa Vicarage Road na kocha wao Mazzarri alikuwa na matumaini nahodha wao huyo angekuwa katika ubora kama alivyofanya wiki iliyopita katika mchezo ambao walishinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Hammers.

Ushindi huu wa kwanza katika michuano ya Ligi Kuu ndicho kilichoongeza presha kwa timu hiyo.

“Lile bao ambalo alilifunga Deeney dhidi ya Westham lilikuwa tamu,” Mazzarri aliiambia Sky Sports.


“Ni wachezaji wachache wanaoweza kufanya hivyo na mmojawao alikuwa ni Maradona. Lilikuwa ni tamu,” aliongeza kocha huyo.

No comments