MWANARIADHA ETHIOPIA ALIYEPINGA SERIKALI AWASILI MAREKANI

MWANARIADHA wa Ethopia na mshindi wa medali ya fedha wa mbio za Olimpiki, Feyisa Lilesa aliyeonyesha alama ya “X” alipomaliza mbio zake, amewasili nchini Marekani.

Hii inatokea takriban wiki tatu baada ya taarifa yake kugonga vichwa vya habari kuhusu alipokunja juu mikono yake kwa alama ya “X” juu ya kichwa chake wakati akimaliza mbio hizo jijini Rio.

Alama hiyo ni ishara ya kupinga serikali inayotumiwa na waandamanaji katika jimbo anakotoka la Oromia na imefanya dunia kutambua wimbi la maandamano nchini Ethiopia.

Feyisa iwapo atarejea nyumbani atakuwa na hofu ya maisha yake ama anaweza kukabiliwa na kifungo cha gerezani kutokana na tendo hilo alilolifanya.

Aliishi nchini Brazil baada ya kushinda medali yake katika siku ya mwisho ya michezo hiyo Agosti 21, ambapo alikataa kurejea nyumbani na timu ya wanariadha wengine wa Ethiopia.

Serikali ya Ethiopia ilisema itampokea nyumbani kama shujaa.

Feyisa alisema kuwa ameadhimia kuomba uhamiaji nchini Marekani.

Kwa sasa yuko mjini Washington DC baada ya kupewa kibali cha dharura cha kuishi nchini humo.

Ukurasa wa mtandao wa kijamii umefunguliwa na Waethopia wanaoishi Marekani kwa ajili ya kutafuta fedha za udhamini wa mahitaji ya maisha yake.


Hata hivyo, ndugu na jamaa zake bado wanaishi nchini Ethiopia.

No comments