MWIGIZAJI VIDYA BALAN WA BOLLYWOOD AKUMBWA NA HOMA YA DENGUE

MWIGIZAJI mahiri wa Bollywood, Vidya Balan amezuiwa kuendelea na utambulisho wa filamu zake mbili mpya baada ya kukumbwa na homa ya Dengue.

Msanii huyo amebainika kuumwa Dengue baada ya kurejea India akitokea nchini Marekani alikokwenda kukamilisha kazi ya kurekodi na kuitambulisha filamu yake ya ‘Kahaani 2’.

“Ni kweli Vidya amesimamishwa kufanya kazi na madaktari kwa siku kumi kutokana na kubainika kukumbwa na homa ya Dengue,” alisema mmoja wa wasaidizi wake.

Filamu mbili mpya za Vidya Balan ni ‘Kahaani 2’ na ‘Begum Jaan’ ambazo hadithi yake na mashahiri yameandikwa na mtaalamu Madhavi Kutty.

No comments