NAY WA MITEGO AKATA SHOO ZA ULAYA ZISIZOMLIPA

NAY wa Mitego amesema kuwa bila kulipwa pesa ya maana hawezi kukubali kwenda nje ya nchi kufanya shoo kama ambavyo baadhi ya wasanii wamekuwa wakienda.

Alisema kuwa wapo wasanii wachache ambao wamekuwa wakipata pesa nzuri kwenye shoo za nje lakini wengi wao huambulia kidogo tu jambo ambalo yeye (Ney) anaona ni sawa na kupoteza muda.

Alisema kuwa amekuwa akipata mialiko mingi lakini huwa anakataa kwa madai kwamba hataki kulipwa pesa kidogo hivyo ataendelea kuwa wa hapahapa na kama ni Ulaya itakuwa ni kwa ajili ya shughuli zake nyingine.


Alidai baadhi ya wasanii wanasema kuwa ni mshamba wa kwenda Ulaya na kudai kuwa hao ndio wanaokwenda kufanya shoo kwenye eneo dogo la uwani na kuonekana wamejaza mashabiki kumbe si chochote.

No comments