NDUGU YAKE IBRAHIMOVIC AKIRI KUWA MBIONI KUSAJILIWA NA REAL MADRID

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Sweden, Alexander ISak ambaye anatajwa kwamba ni “Zlatan Ibrahimovic” mpya, amekiri kwamba anaweza kusajiliwa na Real Madrid ya Hispania. 

Gazeti la Michezo la Swedwen la Aftonbladet limeandika kuwa, uongozi wa timu ya Madrid umeshatuma wawakilishi wake kwenda kuonana na timu ya AIk anayocheza kinda huyo mwenye umri wa miaka 17.


Hata hivyo mchezaji nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic alishakiri kwamba kijana huyo ndiye atakuwa msaada mkubwa kwa Sweden baada ya yeye kutundika daruga. 

No comments