PEP GUARDIOLA AMUHITAJI HECTOR BELLERIN MANCHESTER CITY

WAKATI ikielezwa kuwa beki wa kulia wa Arsenal Mhispanias Hector Bellerin atafuata nyayo za Cesc Fabregas kwa kurudi Camp Nou, sasa anaonekana kuwekwa mtu kati baada ya Pep Guardiora naye kuelezwa anahitaji huduma yake Manchester City.

Makamu wa rais wa Barcelona, Jord Mestre amezungumzia kukua kwa kipaji cha Bellerin hivyo kuongeza tetesi kwamba mabigwa hao wa La Liga watasajili tena.

Bellerin ni zao la Barcelona kutokana na kulelewa katika timu ya vijana ya klabu hiyo na akiwa na miaka 16 alitua mikononi mwa Arsenal Wenger ambapo kwa sasa ana miaka 21.


 “Tayari tumemuona anaipenda [shabiki wa Barcelona],” Mestre alisema katika mahojiano yake na Sport “Ni mchezaji wa kiwango cha juu hakuna hofu kwa hilo.”

No comments