Habari

PICHA 10: CHAZ BABA JUKWAANI TENA TWANGA PEPETA …asema siku zote wanyama wakali hufungiwa

on

MWIMBAJI Chaz Baba ambaye hatma yake na Mashujaa Band bado haijajulikana, Jumamosi usiku alipanda tena jukwaa la bendi yake ya zamani Twanga Pepeta ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ikumbukwe kuwa Mashujaa Band ilishawahi kuipiga mkwara Twanga Pepeta kuwa isithubutu kumpandisha Chaz Baba kwenye majukwaa yake.
Katika mkwara huu uliotolewa kwa maandishi na nakala kwenda kwa Chaz Baba, Mashujaa ikasema agizo hilo likikiukwa basi Twanga na msanii huyo wataburuzwa mahakamani.
Lakini hii inakuwa ni mara ya pili kwa Chaz Baba kupanda jukwaa la Twanga Pepeta ndani ya mwezi mmoja, jambo linaloashiria kuwa Mashujaa wamelegeza uzi wao.
Mara ya kwanza ilikuwa ni Septemba 3 ambapo siku hiyo Chaz Baba aliwasifia mabosi wa Mashujaa kwa kusema: “Namshukuru sana Papaa Maisha na Mamaa Sakina  kwa kunisamehe, nawashukuru kwa kuniruhusu sasa niwe karibu na dada yangu Luizer Mbutu.”
Lakini safari hii Chaz Baba akaibuka na usemi wenye utata kwa kusema: “Siku zote wanyama wakali ndiyo huwa wanafungiwa, lakini wanyama wasio na madhara kama paka huachwa huru.”
Mwimbaji huyo aliimba wimbo wa “Mwana Dar es Salaam” na kama kawaida, akalamba pesa kibao.
Duru za uhakika za kiburudani zilizoifikia Saluti5 zinadai kuwa kabla mwaka huu haujakatika, Chaz Baba atakuwa amerejea Twanga Pepeta.
Chaz Baba akiwa sambamba na Rogart Hegga kwenye jukwaa la Twanga Pepeta Jumamosi usiku
 Hajj BSS na Ferguson wakifanya makamuzi
 Kalala Jr akitupia masauti yake
 Luizer Mbutu na God Kanuti wakifanya yao katika wimbo Mwana Dar es Salaam
 Madansa wa Twanga wakishambulia jukwaa
 Dansa Stella katika ubora wake
 Chaz Baba ndani ya Mango Garden
 Chaz Baba akiimba “Mwana Dar es Salaam”
 Chaz Baba na Kaposhoo
Thabit Abdul naye alikuwepo, akalishika gitaa la kati wakati Chaz Baba akiimba “Mwana Dar es Salaam”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *