PICHA 10: HIZI NDIO RAHA ZA EAST AFRICAN MELODY KILA JUMATANO DAR LIVE


KWA wale wapenzi wa taarab wenye kupenda nyimbo laini ndani sehemu tulivu, basi kundi la East African Melody linaweza kuwa jibu zuri kwao hususan kwa kila siku za Jumatano.

Kundi hilo hupatikana ndani ya ukumbi wa Dar Live pande za Mbagala jijini Dar es Salaam kila Jumatano.

Moja ya raha za Melody ndani ya Dar Live, ni ile hali ya kutumbuiza kwenye jukwaa kubwa na la kisasa sambamba na ‘sound’ bab kubwa inayokupa muziki wenye usikivu murua.

Lakini kingine ni namna ukumbi ulivyo na nafasi ya kutosha inayokufanya upate burudani kwa kujinafasi huku usalama nao ukiwa ni wa hali ya juu.

Pata picha 10 za onyesho la East African Melody Jumatano iliyopita ndani ya Dar Live.
 Abdallah Ng'onda kwenye mpini wa bass gitaa
 Huyu ni mwimbaji Hanifa Juma
 Bi Mwanaidi Shaaban akifanya yake kwenye ukumbi wa Dar Live Jumatano iliyopita
 Hassan Sudi kwenye kinanda
 Mariam Alawi 
 Mussa Makame kwenye gitaa la solo
 Bi Mwanaidi akifanya makamuzi Dar Live
 Ramla akitupia masauti yake
 Safu ya waimbaji wa Melody
Hashim Said akifuatilia onyesho la bendi yake ya nyumbani

No comments