PICHA 10: SIKINDE YAJA KIVINGINE …YAINGIA STUDIO KUIRUDIA “HIBA” YA MWAKA 1985


BENDI ya Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae imeingia studio kuurudia wimbo wake wa zamani “Hiba” uliorekodiwa katikati ya miaka ya 80.

“Hiba” utunzi wake marehemu Muharami Said umerudiwa upya katika studio za Sofia Records jijini Dar es Salaam na umefupishwa hadi kufikia dakika 3:50.

Saluti5 iliyokuwepo katika studio hizo Jumanne jioni, ilishuhudia namna wimbo huo ulivyofupishwa bila kuathiri maeneo nyeti ya wimbo.

Magitaa manne yamepigwa humo ndani ambapo gitaa la kati limepigwa na Mjusi Shemboza, bass limepigwa na Juma Amir, solo akasimama Kaingilila Maufi huku second solo likikung’utwa na Shehe Kombo.

Tumba zikapigwa na Ali Jamwaka huku saxophone likipulizwa na Shaaban Lendi wakati kwenye uimbaji ameongoza Hassan Bitchuka kwa kuitikiwa na Abdallah Hemba na Said Mussa Msakara.

Ni wimbo mtamu ambao unachezeka kuanzia mwanzo hadi mwisho na ni wazi kuwa utakuwa changamoto nzuri ya bendi zetu kuzirudia tungo zao za dhahabu katika studio za kisasa na kwa kuzingatia soko la sasa. Wimbo unatarajiwa kuwa hewani mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo.
 Abdallah Hemba akinogesha wimbo wa "Hiba" kwa sauti zake za chini
 Hassan Rehani Bitchuka akitupia sauti zake tamu
 Ali Jamwaka akizigonga tumba
 Juma Amir akasimama vizuri kwenye bass gitaa
 Kaingilila Maufi kwenye solo gitaa
 Shaaban Lendi akipuliza saxaphone 
 Mjusi Shemboza kwenye gitaa la rhythm
 Producer Ababuu mwana Zanzibar 
 Mwimbaji chipukizi wa Sikinde Said Mussa Msakara 
Shehe Kombo akipapasa mpini wa second solo

No comments