PICHA 10 ZA ONYESHO LA KWANZA LA HUSSEIN JUMBE BAADA YA LIKIZO YA MARADHI …aibuka na wimbo “Kipima Joto”


JUMATANO usiku mwimbaji mahiri wa muziki wa dansi, Hussein Jumbe alipanda kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa la bendi yake ya Talent baada ya kupona maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Hiyo ilikuwa ni ndani ya ukumbi wa Bulyaga uliopo Temeke ambapo mashabiki wa muziki wa dansi walionekana kupagawa kwa furaha baada ya kumuona Jumbe jukwaani.
Kwa zaidi ya miezi miwili Hussein Jumbe alikuwa hoi kitandani hali iliyomfanya asionekane  jukwaani na kupelekea Talent Band kufanya maonyesho bila uwepo wake.
Jumbe akionekana mwenye afya njema, akatesa na nyimbo zake maarufu kama “Siri ya Nini”, “Nachechemea” na “Kiapo Mara Tatu”.
Kama vile hiyo haitoshi, Jumbe akaibuka na wimbo mpya kabisa “Kipima Joto” ambao maudhui yake hataofautiani sana na “Nachechemea”.
Katika “Kipima Joto” Jumbe anaelezea kiaina juu ya kuugua kwake na namna baadhi ya watu walivyooibuka na uvumi wa kila aina juu ya maradhi yake.
Pata picha 10 za onyesho hilo la Talent Band chini ya Hussein Jumbe.
 Fadhil Ally akikung'uta gitaa la solo
Hussein Jumbe akicheza na mashabiki wake 
Hussein Jumbe akiiimba sambasamba na mkewe ambaye ni shabiki namba moja wa Talent Band 
 Mtu na mtuwe
Jumbe akiimba wimbo mpya "Kipima Joto"
 Hussein Jumbe akiimba kwa hisia kali
 Hussein Jumbe
 Saad Ali katika drum
Asia mmoja wa waimbaji wa Talent Band
No comments