Habari

PICHA 17: JOSE MARA MOTO CHINI NA MAPACHA MUSIC BAND …tupia macho mastori na mapicha ya show yao ya Meridian Kinondoni

on

JOSE MARA amedhihirisha ubora wake kwa kuliongoza vema kundi la
Mapacha Watatu ambalo kwa sasa linajulikana kama Mapacha Music Band.
Jumapili usiku Saluti5 ilitembelea onyesho la bendi hiyo katika ukumbi
wa Meridian Hotel (Club Masai) Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukutana na
muziki uliokwenda shule.
Kinyume na watu wengi walivyodhani kuwa bendi ingeyumba baada ya
kuondoka kwa Khalid Chokoraa aliyerejea Twanga Pepeta, lakini Mapacha ndo kama
imeongezewa kasi.
Ikiwa na nyongeza ya waimbaji kadhaa akiwemo Cantona aliyepata kutamba
na Dimond Musica, Mapacha ikafanya makamuzi ya kufa mtu huku ikiwa na vyombo
vipya kabisa.
Jose Mara akaonyesha ufundi wake wa kucheza na sauti katika uimbaji
wake uliowavutia wengi, lakini pia alitesa kwenye upande wa rap akisaidiana na
Titilaa.
Upande wa wapiga vyombo bendi hiyo ilionyesha ubabe wa kupangilia
muziki mzito chini ya mpiga drum anayekulikana kama Computer Drums pamoja na mkali
wa kinanda Erasto Mashine, achilia mbali mpiga solo Super Black.
Mwimbaji wa FM Academia King Blaise aliyekuwepo ukumbini hapo,
alikwenda jukwaani kusalimia kisanii na kuimiminia sifa nyingi bendi hiyo
hususan kwa Jose Mara na Computer Drums.
Pata picha 17 za onyesho hilo huku ukikumbuka pia kuwa Mapacha
wanakuwepo Meridian kila Jumapili.
 Jose Mara (kushoto) akimkaribisha jukwaani King Blaise wa FM Academia
 Cantona akitupia sauti za hatari 
 Computer Drums alitisha sana kwenye drums
 Erasto Mashine akikipapasa kinanda
 James akikung’uta bass gitaa
 Jimmy Gola mmoja wa waimbaji nguzo ya Mapacha Music Band
 Jose Mara na King Blaise wakikumbushia enzi za Ngwasuma 
 Waimbaji wa Mapacha na madansa wao wakishambulia jukwaa
 Jose Mara akitupia sauti zilizojaa hisia kali
 Said Kombola akifanya yake kwenye gitaa la kati
 Sammy John namba nyingine hatari kwenye safu ya uimbaji ya Mapacha
 Super Black na solo lake
 Rapa Titilaa
Jose Mara
 Vincent kwenye bass
 Waimbaji wa Mapacha wakitupia masauti yao matamu
Mwimbaji wa Mapacha Catherine Chuma akiwa na meneja wa bendi Aristide Rubeya

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *