Habari

PICHA 17 ZA MAKAMUZI MAKALI YA TWANGA PEPETA IDD MOSI VIJANA SOCIAL HALL

on


BENDI ya The African Stars “Twanga Pepeta” siku ya Idd Mosi ilifanya makamuzi makali ndani ya ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni.
Twanga ikiwa na nyota wake wote, ikapiga bonge la show lililosuuza nyoyo za mashabiki wao.

Bendi hiyo ikaweka kipengele cha madansa wao wa kiume kujaribu kuonyesha vipaji vya kurap, kitu ambacho kiliongeza msisimko mkubwa wa onyesho hilo ambapo baadhi yao walitisha kwa umahiri wao huku wengine wakigeuka kituko na kuwavunja mbavu mashabiki.
 Khalid Chokoraa akifanya yake
 Madansa wa kike wa Twanga wakipagawisha mbele ya mashabiki wao
Madansa wa Twanga katika ubora wao
 Ferguson akishambulia jukwaa
 Hajj BSS akiimba kwa mbwembwe za hali ya juu
 Hosea akipaga bass gitaa kwa hisia kali
 Kalala Jr jukwaani
 Godi Kanuti kwenye gitaa la kati
 Kaposhoo ‘akizikomesha’ tumba zake
 James Kibosho kwenye drum
 Luizer Mbutu akionyesha umahiri wake wa uimbaji
 Hajj Bss akishuka chini kwenda kuwapagawisha mashabiki
 Khalid Chokoraa (kushoto) na Rogart Hegga
 Miraji Shakashia na gitaa lake la solo
Dansa Stela katika ubora wake
Madansa wa kiume wakishambulia jukwaa
Victor Nkambi akipapasa kinanda

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *