PICHA 7: CHOKORAA ALIVYOIANZISHA SHOW YA TWANGA PEPETA MANGO GARDEN USIKU HUU


KAMA ambavyo Saluti5 iliwahi kusema siku za nyuma, Khalid Chokoraa si wa kawaida linapokuja suala la kuwahi kazini.

Jamaa hanaga ustaa, mapema sana alikuwa ndani ya Mango Garden na ilipotimu saa 3:30 usiku akapanda jukwaani na kuanza kungurumisha burudani akiwa mwimbaji pekee stejini.

Alifanya hivyo hadi saa 4:20 kabla hawajapanda waimbaji wengine kuendeleza program ya onyesho hilo linaloendelea usiku huu ndani ya Mango Garden.


Pata picha 7 saba.
 Khalid Chokoraa jukwaani Mango Garden
 Khalid Chokoraa 
Hosea akipiga gitaa la bass kwa mbwembwe
 Kanuti kwenye mpini wa solo
James Kibosho akizigonga drum
Victor Nkambi kwenye kinanda
Khalid Chokoraa akithibisha kuwa muziki unawasubiri wateja na sio wateja kusubiri muziki

No comments